Serikali imejipanga katika kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuboresha miundombinu  ili kuenda na kasi ya ukuaji wa teknolojia.

Hayo yamebainishwa na  Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrew Mathew leo Februari 25 alipokutana na Wankandarasi wa miundombinu ya mawasiliano, watoa huduma za mawasiliano na wabunifu ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumza katika mkutano huo, Kundo amesema kuwa Serikali ipo tayari kutatua changamoto zinazowakabili katika ubunifu na TEHAMA ikiwemo changamoto ya mikataba inayosainiwa kukamilika kwa muda mrefu.

Kundo ameainisha changamoto inayowakabili wabunifu ya kutofaidika na ubunifu wao na kusema kuwa serikali ipo tayari kutatua changamoto hizo huku wakishirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH huku akiwashauri wabunifu kujisajili kwenye TEHAMA .

Kundo amesema kuwa sasa wakati umefika kwa mawasiliano kuwa njia ya pili kukuza uchumi wa nchi kwa kushirikiana na wabunifu mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi (COSTECH), Amos Nungu amesema kuwa kwa upande wa Tume mkutano huo ni muhimu kwani kupitia mkutano huo watajidialiana na kujenga msingi  mzuri katika kujenga uchumi wa kidigitali

Aidha Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Justine Mashiba amesema kuwa mpaka kufikia sasa wamesaini mikataba ya kupeleka huduma za mawasiliano katika kata 1057 na vijiji 3792 na miradi inatarajiwa kumalizika Oktoba 2021.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 26, 2021
Rais Magufuli asisitiza matumizi sahihi ya mitandao