Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule amekutana na wafanyabiashara kwa lengo la kujadili changamoto za biashara kwa ujumla na kuweka maazimio yenye tija katika kukuza masoko kwa kutumia fursa zilizopo  ndani na nje ya nchi.

Senyamule amekutana na Wafanyabiashara hao, jijini Dodoma ambapo wafanyabiashara wakubwa, wakati na wadogo wakiwemo viongozi wa masoko, wamiliki wa shule, wamiliki wa Nyumba za wageni, Viongozi wa makampuni mbalimbali, wauza vipodozi na wafanyabiashara wa Mbao, walihudhuria.

Mbele ya kadamnasi hiyo, Senyamule alisema”sisi Mkoa wa Dodoma tuna dhamira ya kuhakikisha wafanyabiashara wanakaa katika Mazingira mazuri na tunajipanga kufanyia kazi changamoto na maazimio ili kuendelea kuboresha huduma katika nyanja zote.”

Awali, wafanyabiashara walitoa changamoto mbalimbali zinazowakabili ndani ya masoko zikiwemo ulipishwaji wa kodi ya pango ikiwa siyo wamiliki wa nyumba, wingi wa kodi kwa wafanyabiashara, ubovu wa miundombinu ikiwemo barabara,   upungufu katika kaguzi za risiti, mfumo wa ulipaji kodi usio rafiki na changamoto za uzoaji wa taka na maji taka.

Bellingham, Real Madrid mambo Bam Bam
Ufuatiliaji miradi, shughuli za Serikali wajadiliwa