Serikali imepanga kuweka sharti la kuwasilisha mche mmoja wa mti shuleni kwa wanafunzi wote watakaoandikishwa darasa la kwanza na miche mitatu ya mti kwa watakaojiunga na kidato cha kwanza kwa shule zote za serikali na binafsi. ‘

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, alipokuwa akishirikia zoezi la upandaji miti na wanafunzi wa shule ya msingi Mlandege iliyopo katika Manispaa ya Iringa.

Akiongozana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa katika zoezi hilo, Makamba alisema kuwa wizara yake itashirikiana na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha sharti hilo linazingatiwa ipasavyo.

Makamba akipanda Mti

aziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba

Alisema kuwa moja kati ya mahitaji ya kupewa cheti cha kuhitimu darasa la saba na kidato cha nne, kukabidhi mti uliopandwa na kutuzwa na mwanafunzi tangu alijiunga na masomo ya cheti husika.

Aidha, Waziri Makamba ameainisha kuwa katika shule zenye uhaba wa maeneo yanayoweza kutumika kwa upandaji miti, maeneo mbadala yatakayoelekezwa na serikali za vijiji na mitaa.

“Hii ni moja kati ya hatua mahsusi, stahiki na za maksudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuendana na mabadiliko ya tabia nchi hasa ikizingatiwa kuwa asilimia 61 ya nchi yetu ipo katika tishio la kuwa  jangwa,” alisema Makamba.

Katika hatua nyingine, Makamba alisema kuwa Wakuu wa Wilaya zote, Wakurugenzi na Wenyeviti/Mameya wa halmashauri watahudhuria mafunzo maalum jijini Arusha kuanzia Novemba 5 mwaka huu kuhusu uhifadhi bora wa mazingira na kampeni ya upandaji miti.

Jaji Lubuva aomba wananchi kutoa ushirikiano elimu ya mpiga kura
Video: Ziara ya Waziri Maghembe yaibua madudu chuo cha Utalii