Serikali ya Gambia imepanga kupiga mnada ndege za kifahari pamoja na magari ya rais wa zamani wa nchi hiyo , Yahya Jammeh kwa njia ya mtandao.

Nchi majirani waliingilia kati kumtimua madarakani Rais Jammeh baada ya kushindwa kwenye uchaguzi Disemba mwaka 2016 ambapo alikataa kuondoka madarakani.

Aidha, Jammeh aliacha ndege tano na magari 30 ya kifahari, yakiwemo ya Rolls-Royce na Bentley pamoja na mashamba manne.

Hata hivyo, Mwaka jana serikali ya nchi hiyo ilisema kuwa ina nia ya kupata mamilioni ya dola kutokana na kuuzwa kwa mali za Jammeh na kuwekeza fedha hizo katika sekta za afya na elimu.

 

 

Ajali mbaya yatokea Mbeya ikihusisha Lori na Hiace tatu za abiria
Video: Lissu atoboa siri ya dereva wake, Tajiri awatwanga risasi maofisa usalama taifa