Serikali ya Kenya imetangaza kupitia gazeti la serikali kuwa kesho itakuwa siku ya mapumziko kusherehekea Siku Kuu ya Eid al Fitr.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i ameeleza kwenye tangazo hilo kuwa ameitangaza siku hiyo kwa mamlaka aliyopewa na katiba ya nchi.

“Ninapenda kuueleza umma kuwa kwa kuzingatia Kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, ninatangaza kuwa Jumatano, Juni 5, 2019 itakuwa siku kuu ya umma kwa ajili ya kusherehekea siku ya Idd al Fitr,” limeelza tangazo hilo.

Kwa mujibu wa kalenda, Tanzania pia inatarajiwa kuitangaza siku ya kesho kuwa sikukuu ya Eid al Fitr, ambapo waumini wa dini ya Kiislam wanatarajia kuuona mwezi ukiandama leo jioni.

Sikukuu hii huadhimishwa duniani kote kufuatia siku 30 za mfungo unaoambatana na sala za toba na kujitolea kama inavyoelekeza Quran Tukufu.

Video: Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa, Dkt. Mpango awasilisha bajeti ya trilioni 11.9
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 4, 2019