Serikali ya Kenya imeamua kutumia njia ya mazungumzo kumaliza mgogoro kati yake na viongozi wa vyama vya upinzani kufuatia maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa upande huo kushinikiza kujiuzulu kwa Tume Huru ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini humo.

Maandamano

Taarifa zilizotolewa na Ikulu ya Nairobi zimeeleza kuwa Rais Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga pamoja na kiongozi wa upinzani Bungeni, Seneta Moses Wetangula.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikuelezea kwa undani mazungumzo yaliyofanyika kati ya viongozi hao na maamuzi yaliyofikiwa.

Hivi karibuni, yalizuka maandamano makubwa nchini humo kushinikiza Tume ya Usimamizi wa Uchaguzi (Electoral and Boundaries Commission (IEBC) kuondolewa kwa kuwa na upendeleo katika utendaji wake. Watu watatu waliripotiwa kupoteza maisha katika mapambano kati ya waandamanaji na Jeshi la Polisi wiki iliyopita.

Kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Agosti 2017.

Mbeya City Kufanya Ziara Nchini Malawi
Mourinho: Sitathubutu Kupoteza Muda Kwa Kumfikiria Pep Guardiola