Serikali ya Kenya kupitia Waziri wa afya Mutahi Kagwe imetishia kuwafuta kazi wahudumu wa afya walioamua kugoma wakilalamikia stahiki zao mbali.

Kwa miezi kadhaa sasa madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali za umma nchini Kenya  wameungana na wahudumu wengine kwenye mgomo kulamamikia kutopewa bima ya afya na kufanya kazi kwenye mazingira magumu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia changamoto ya janga la Covid-19.

Mgomo huu unakuja baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa Madaktari na serikali nchini humo kugonga mwamba wa wakati huu nchi nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na janga la Corona.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 94,500 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 349 kuthibitishwa na vifo 94,500 baada ya ya watu wengine 6 kuthibitishwa kufariki dunia kutoka na janga hilo hatari la COVID-19.

Watu 176 wameripotiwa kupona virusi hivyo na kufanya idadi ya jumla ya watu waliopona kufikia 75,735.

Maonyesho ya kilimo biashara kuwakutanisha wakulima zaidi ya 4,000
Manula, Bocco waivuruga Simba SC Harare