Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imeazimia kuanza zoezi la kuwapima vinasaba (DNA) watoto wa mitaani ili kubaini wazazi wao halisi.

Akizungumza jana na Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za Kulevya, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alisema kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza watoto wa mitaani.

Profesa Manyele alisema kuwa kumekuwa na idadi kubwa ya watoto wa mitaani jambo ambalo inawezekana limetokana na familia zenye uwezo kuwatelekeza watoto hao baada ya kushindwa kuwapa malezi.

Alisema kuwa zoezi la kufunga mitambo na vifaa vingine unaendelea na kwamba upimaji huo utaanza kufikia Julai mwaka huu.

Exclusive: Jaffarai aeleza Magufuli alivyomvuta kuingia kwenye siasa, Ushauri wa Kufanikiwa Kibiashara na muziki wake (Audio)
Makonda achota baraka kuisafisha Dar