Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  ametoa miezi mitano kwa maduka binafsi ya dawa yaliyo nje ya Hospitali au vituo vya kutolea huduma za afya nchini yawe umbali wa Mita 500 Kama kanuni ya mwaka 2020 ya uanzishaji wa maduka ya dawa inavyoelekeza.

Imeelezwa kuwa maduka hayo yapo kinyume cha kanuni ya famasia iliyowekwa mwaka 2020 hivyo wamiliki watachukuliwa hatua za kisheria.

“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.

“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameyasema hayo baada ya kukutana na malalamiko ya ukosefu wa dawa kutoka kwa wagonjwa hospitalini hapo.

“Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,” amesema Waziri Ummy

TFF yakanusha kumfungulia kesi Barbara
Pablo awapongeza wachezaji Simba SC