Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema Wizara katika kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzingatia maoni na ushauri wa Kamati ya Bunge imeanzisha Kitengo cha usimamizi wa majengo ambacho kitakuwa chini ya Mkurugenzi msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Amesema pamoja na kuanzishwa kwa Kitengo hicho Wizara imeendelea kushirikiana na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakifuata sheria na taratibu zilizopo.

Ameeleza kuwa uamuzi wa kuanzishwa kwa kitengo hicho unatokana na ushauri uliotolewa na Kamati hiyo uliyoitaka Wizara kuhakikisha mipango ya ujenzi wa majengo ya ofisi na makazi ya Balozi mbalimbali nje ya nchi unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi mkubwa.

“Uamuzi huu umetokana na ushauri ambao Kamati hii iliutoa kwa Wizara katika kuhakikisha suala la ujenzi wa majengo ya Balozi zetu unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi,” alisema Prof. Kabudi.

Waziri amesema Wizara inaendelea na mipango ya kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika mipango na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchininikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia maendeleo na kusaidia ndugu na jamaa zao waliopo nchini.

Pia kufanya uchambuzi wa mazingira ya ushirikishwaji wao na kuangalia masuala ya kisheria, kitaasisi ushirikiano na sekta binafsi takwimu za Watanzania waishio ughaibuni na uwezo na hamasa ya kuchangia maendeleo ya nchi.

Nugaz aitaka Simba SC ASFC
Corona yapita na wachezaji tisa FC Sion