Mganga mkuu wa Serikali prof. Abel Makubi mapema leo amebainisha makundi matatu ya watu ambao watafanyiwa majaribio ya dawa dhidi ya homa kali ya mapafu iliyotoka Madagascar pamoja na ile iliyotengenezwa Tanzania.

Amesema baada ya kupokea dawa kutoka Madagascar, hawataanza kuwapa moja kwa moja watanzania bila kufanyiwa majaribio kama ipo salama japo serikali ya madagascar imeshafanya tafiti.

Amebainisha makundi matatu ya watu ambao watafanyiwa utafiti kuwa ni wagonjwa ambao wataendelea kutumia dawa ya madagascar pamoja na dawa wanazotumia sasa.

Na kundi la pili ni la wagonjwa ambao wataendelea na dawa za awali lakini watapewa dawa iliyotengenezwa Tanzania na kuthibitishwa na NIMR.

Kundi la tatu ambalo pia ni wagonjwa waliokubali kwa hiari yao ambao wataendelea kutumia dawa ambazo zimekuwa zikitumiwa awali ili kujua ufanisi wa dawa mpya.

Aidha amebainisha kuwa Tanzania haiwezi kujiteka katika tafiti dhidi ya vita ya corona hasa katika suala la kutafuta dawa na kutolea mfano kuwa kunadawa ambayo imeonesha matumaini Marekani ambayo Tanzania inaifuatilia.

Uganda: Madereva wazidi kuongeza visa vya Corona, Museveni atangaza maombi
Waziri Kabudi amesema hawana dawa za kugawa, utafiti kwanza