Fundi Seremala mmoja nchini Kenya ameishtaki serikali akidai kutaka kulipwa $2m (£1.5m) malipo ya viti viwili alivyomtengenezea rais mstaafu Daniel Arap Moi miaka 26 iliyopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Nairobi News’ nchini humo, Solomon Njoroge Kiore amesema kuwa aliwasilisha viti hivyo kwenye ofisi ya maonyesho ya kilimo ya Nairobi kwa hafla ya rais ya siku tatu.

Aidha, Mtandao huo wa habari umeripoti kuwa mawakili wa serikali walidai mwezi Februari kwamba waliafikiana kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama lakini hawajawasiliana tena na Kiore tangu wakati huo.

“Rais Mstaafu, Daniel Moi alivitumia viti hivyo kwa mwaka mmoja, kabla ya viti hivyo kurudishwa kwangu”, amesema Kiore

Hata hivyo, Kiore ameongeza kuwa angependelea viti hivyo kuwekwa katika jumba jipya la makumbusho lililopo katika Ikulu ya rais.

 

 

Diamond athibitisha kumnunulia Hamisa ghorofa
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Tunisia