Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Leonard Subi amesema serikali imechukua hatua mbalimbali za kupambana na Covid-19, ikiwemo kuimarisha mifumo ya utoaji huduma za afya kama vile kusimika mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya oksijeni na utoaji wa chanjo dhidi ya janga hilo.

Amesema hayo mbele ya waandishi wa habari Mkoani Mwanza wakati akizindua mkutano wa elimu kuhusu umuhimu wa utoaji chanjo ya Covid-19 nchini.

Dkt. Subi amesema wameimarisha miundombinu ya utoaji huduma za afya katika hospitali ikiwemo upatikanaji wa hewa tiba ya oksijeni.

Aidha ameeleza kuwa awali suala la oksijeni nalo lilikuwa changamoto lakini katika mlipuko huo wameendelea kuimarisha miundo mbinu hiyo.

“serikali hii ya awamu ya sita tumesimika mitambo mipya ya uzalishaji wa hewa ya oksijeni katika hospitali za rufaa za Mikoa, na kila mtambo unaweza kuzalisha mitungi 200 ya oksijeni kwa siku na wakati.” Amesema Dkt. Subi.

Ameeleza kuwa hivi sasa wanaendelea na usimikaji wa mitambo katika hospitali za Mikoa za Rufaa, baadhi ya Wilaya na kanda, pia serikali imetoa bilioni 10 kwaajili ya kuahakikisha huduma kwa wananchi.

Biteko: usalama ni jambo muhimu katika maeneo ya kazi
Afghanistan:Sheria mpya kwa wanafunzi wa kike