Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Ndalichako amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa inawajengea ujuzi vijana ili ukawe manufaa kwa jamii inayowazunguka hivyo amewataka kutokata tamaa kwani wanashiriki katika kujenga nchi kwa bunifu zao zenye tija.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.

“Vijana wanahitaji kuaminiwa tunahitaji tuwape fursa, vijana wetu wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo  tusiogope kuwakaribisha tuwape nafasi ili waweze kuonesha ujuzi wao”. Amesema Prof.Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu amesema wamekuwa wakiwafuatili vijana ambao wamepitia mafunzo ya ubunifu kwani lengo lao ni kuwasaidia wabunifu ili waweze kuonyesha mchango wao katika jamii.

Senzo: Young Africans msijisahau
Simba Queens mguu sawa CECAFA