Leo Juni 21, 2018 Serikali imepokea Sh1 Bilioni kama gawio la faida la Shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) zilizotokana na faida ya Sh28.5 bilioni baada ya kupata faida ya sh29.2 bilioni kabla ya kukatwa kodi katika shirika hilo.

Gawio la fedha hizo limetolewa mbele ya Rais John Magufuli wakati wa hafla fupi ambapo ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema makubwa yalianza kuonekana kupitia uongozi wa awamu ya tano.

Kwa mara ya kwanza shirika ilipanga kutoa Tsh 1 bilioni kwa serikali ila mara baada ya kuona biashara inaendelea vizuri likaona ni vyema kuongeza faida hiyo kwa Serikali.

”Tuliahidi kutoa gawio la Sh1 Bilioni lakini baada ya bodi ya Shirika kukaa ikaamua kuongeza gawio hilo baada biashara kwenda vizuri” amesema Kindamba.

Kindamba ameongezea kuwa katika juhudi za kuimarisha shirika hilo, wameanza kutekeleza maagizo ya serikali baada ya kupunguza safari za nje kwa watendaji wake na kufuta mikataba mibovu isiyokuwa na manufaa kwa shirika.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omar Nundu huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kwa njia ya Teknolojia ya mawasiliano ya video moja kwa  moja Kutoka Dodoma.

Aidha Rais Magufuli amelitaka Shirika hilo kuhakikisha linakusanya vyema madeni kwa wateja wake na kwa mafanikio hayo makubwa waliyoyapata ameamuru wafanyakazi kupandishiwa mishahara.

 

Msigwa akerwa wanaosifia kukua kwa uchumi, amvaa Mpango
Trump asitisha amri inayozitenganisha familia