Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kugawa bure kwa wananchi sukari zilizofichwa na zilizoingia kimagendo nchini.

TRA mkoani Lindi hivi karibuni wamegawa kilo 132,975 za sukari ya Brazil iliyokamatwa ikiingizwa nchini kimagendo kupitia bandari ya Lindi mwezi Februari mwaka huu.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo allisema kuwa baada ya kukamata sukari hiyo waliamua kuigawa kwa taasisi zenye uhitaji maalum zikiwemo kambi za wazee, shule maalum, magereza na vyuo mbalimbali vya umma nchini, baada ya kukaguliwa na Mamlaka ya Chakula na dawa na kubainika kuwa inafaa kwa matumizi ya binadamu.

Sukari hiyo ilikamatwa ikiwa imefungwa kwenye mifuko 5319 yenye ujazo wa kilo 25 kila mmoja.

Michel Platini Akubali Kuachia Ngazi UEFA
Chadema waanza kushikana Uchawi