Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri rasilimali za vyama hivyo na kwamba Serikali haitalipa deni lolote lililokopwa na vyama hivyo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara pamoja na wadau wa zao la kahawa baada ya kuwasili mjini Bukoba kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Amesema kuwa Serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao si waaminifu na wabadhilifu wa mali za ushirika.

Aidha, Majaliwa amepiga marufuku wafanyabiashara kuwaibia wakulima kwa kununua kahawa mbichi ikiwa shambani maarufu kama butura.

“Biashara ya kununua madeni yaliyokopwa na vyama vya ushirika haipo kwenye Serikali hii ya awamu ya tano, badala yake itawachukulia hatua wote waliohusika na ubadhilifu huo.”

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali itahakikisha wafanyabiashara wote, hususani wa mazao ya kilimo wanakuwa na mfumo sahihi wa ununuzi wa mazao utakao ongeza tija kwao na kwa wakulima.

 

Mwigulu Nchemba afunguka kuhusu milioni 50 za kila kijiji
Video: Mama atoa simulizi ya kusikitisha

Comments

comments