Serikali imeahidi kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya kambi ya jeshi la Majimaji na JKT dhidi ya wakazi wa kata ya Kilimahewa Mchonda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kilimahewa, viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea na viongozi wa vikosi vyote viwili ambavyo vimeingia katika mgogoro na wananchi hao.

Amesema kuwa hayo yamefikiwa baada ya kuzipata ripoti zilizotolewa na tume zilizoundwa kwa ajili ya kutatua mgogoro huo ulioanza tangu mwaka 1978.

”Natambua mgogoro huu na kupitia tume tatu ambazo ziliundwa kwa ajili ya kuutatua ikiwemo tume ya wilaya, mkoa na ya Kamishina wa ardhi wa kanda na baadhi ya ripoti bado sijazipata, hivyo nikizipata nitalifanyia kazi’’ Amesema Waziri Mwinyi.

Hata hivyo, Waziri Mwinyi ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kutoruhusu malipo ya korosho zinazodhaniwa kuwa zimechukuliwa na baadhi ya wanajeshi kutoka kwa wananchi waliojenga ndani ya kambi za jeshi ambazo awali ilionesha kuwa zitamilikiwa na kikosi,lakini baadae ikaonekana inabidi zilipwe kwenye akaunti binafsi.

Majaliwa azitaka bodi za mazao kujisajili GS1
Ghana yaongoza kutengeneza majeneza yenye mvuto, yatazame hapa