Rais Magufuli ameahidi kutoa shilingi Bilioni 3.7 ndani ya wiki mbili kwa wafanyakazi wa kampuni ya meli ya Marine Service.’

Ameahidi hayo leo wakati akihutubia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Meli mpya na chelezo katika Ziwa Victoria ujenzi unaogharimu Bilioni 88.

Wafanyakazi hao wanaodai malimbikizo ya mishahara ya takribani miezi 27 wamehimizwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi vinginevyo watazitapika fedha hizo.

Pia amautaka uongozi wa MSCL kufanya marekebisho ya kiutendaji na kuongeza tija ili kumudu kujiendesha kwa faida.

Aidha, Magufuli amempandisha cheo Kaimu Meneja wa Kampuni ya huduma za Meli (MSCL), Erick Hamis kuwa Meneja mkuu kwa kile alichodai kuwa amependezwa na mikakati yake inayoonyesha dhahiri nia yake ya kulifufua shirika hilo na kumpa sharti la kutolewa sifa na kuliua tena shirika.

 

Video: Kama mmeshindwa kutii sheria za nchi ondokeni- DC Muro
Video: JPM awapa tano wabunge CCM, awapiga dongo upinzani