Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) imeendelea kuboresha huduma za afya nchini baada ya leo Agosti 2, 2021 kukabidhi boti mbili mpya MV. Nzera na MV. Ukeree 11 za kubeba wagonjwa (Ambulance Boats) kwa wakazi wa visiwa vya Ukerewe Mkoani Mwanza na Geita vijijini.

Aidha Boti hizo mbili, MV. Nzera itakayokuwa inatoa huduma Geita vijijini na MV. Ukerewe II itakayopelekwa visiwa vya Ukerewe, kila moja imegharimu shilingi milioni 276.6.

Akizungumza wakati wa kupokea Boti hizo katika hafla fupi iliyofanyika katika Yadi ya Songoro iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ujenzi wa boti hizo.

Hali kadhalika RC Gabriel ametoa maelekezo kwa halmashauri husika kuzisimamia na kuziendesha kwa weledi, huku akiitaka TEMESA kushirikiana na Halmashauri kwa kutoa ushauri wa kitaalam mara kwa mara ili boti hizo ziweze kudumu na kuendelea kutoa huduma iliyokusudiwa ya kuwaondolea adha ya usafiri wagonjwa wa maeneo haya.

Sambamba na hayo Serikali pia imepokea Boti ya uokozi, MV.SAR IV yenye wa uwezo wa tani 3, urefu wa mita 11.5, upana wa mita 3 ambayo ilikuwa ikifanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu shilingi milioni 576 kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza.

Pichani ni Boti tatu, MV. NZERA, MV.SAR IV Pamoja na MV. UKEREWE II Kazi Iendelee mara baada ya kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel. Boti mbili za kubeba wagonjwa zimegharimu jumla ya shilingi Milioni 553, wakati boti ya uokozi ukarabati wake ukigharimu shilingi milioni 576.
Picha ni (Ambulance Boat) Boti ya MV. UKEREWE itakayokuwa ikitoa huduma ya kubeba wagonjwa katika visiwa vya Ukerewe. Boti hiyo iliyozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel imegharimu kiasi cha shilingi milioni 217.
Picha ni (Ambulance Boat) Boti ya MV. NZERA itakayokuwa ikitoa huduma ya kubeba wagonjwa Geita vijijini. Boti hiyo iliyozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel imegharimu kiasi cha shilingi milioni 217.

Ambokile anarudi Mbeya City
Mapya yaibuka Rubby na Mosse Iyobo