Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefanikiwa kukamilisha mkakati wa kitaifa wa magonjwa yasiyoambukiza wa mwaka 2013-2020.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukizwa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Profesa Ayoub Magimba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Magimba amesema kuwa mkakati huo ni muendelezo wa utekelezaji wa maazimio ya vikao cha 66 na 68 vya Umoja wa Mataifa vilivyofanyika mwaka 2015 na 2016 ambapo Tanzania iliridhia kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

“Katika kuimarisha huduma za kinga kwa magonjwa hayo, Serikali inatoa elimu kwa wananchi na kuwa himiza kufanya mazoezi, kupunguza matumizi mabaya ya pombe na sigara na kuhamasisha upimaji wa afya angalau mara mbili kwa mwaka,” amesema Profesa Magimba.

Profesa Magimba aliyataja magonjwa yasiyoambukiza kuwa ni pamoja na Saratani, magonjwa ya Moyo, magonjwa sugu ya njia ya hewa, Selimundu, magonjwa ya akili, Figo, Kisukari na baadhi ya magonjwa ya macho.

Takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni tatizo la kimataifa ikijumuisha nchi za Afrika na nchi zinazoendelea.  Magonjwa hayo yamesababisha vifo million 36 duniani sawa na asiliamia 63 kwa kipindi cha mwaka 2008

Waigizaji Marekani kuandamana mara baada ya Trump kuapishwa
Sanamu ya Lionell Messi yavunjwa