Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na gazeti moja la kila siku la Kiingereza pamoja na vyanzo vingine mitandaoni kuwa nchi 14  wadau wa maendeleo wa nchi za Magharibi zimekataa kuipa msaada serikali ya Tanzania kutokana na mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Fedha na Mipango iliyolenga kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo za kunyimwa misaada, ilisema kuwa nchi hizo zinaendelea kutoa misaada kupitia Bajeti Kuu (General Budget Support, Mifuko wa ‘Busket Fund’ pamoja na msaada wa moja kwa moja kwenye miradi (Direct Projects Fund).

Imeeleza kuwa nchi kadhaa kupitia mashirika mbalimbali ya kutoa misaada tayari yameshathibitisha kutoa misaada yake kuchangia Bajeti Kuu. Baadhi ya mashirika hayo ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dernmark, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.

Wizara ya Fedha na Mipango imeeleza kuwa kwa ujumla, nchi zilizothibitisha kuchangia Bajeti Kuu ni pamoja na Marekani, Canada, Ubelgiji, China, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, India, Ireland, Italia, Japan, Korea Kusini, Norway, Sweden, Netherlands na Uingereza.

Hivi karibuni, Shirika la Changamoto za Melenia (MCC) la Marekani lilitangaza kusitisha msaada wa shilingi trilioni 1.3 kwa Tanzania kutokana na kutoridhishwa na uamuzi wa Tanzania kufanya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, pamoja na namna ilivyotekeleza Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015.

Kikosi Cha Al Ahly Kuwasili Kesho
Gardner G Habash arejea Clouds Fm