Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imekanusha kuhusu takwimu zilizotolewa na gazeti la Habari Leo zilizokuwa zikisema kuwa wasichana 2,892 waliokuwa wanafunzi wa shule za msingi wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa walikatishwa masomo yao kutokana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni kwa kipindi cha mwaka 2016.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Mary Siyame imesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2016 jumla ya watoto 9,723 waliandikishwa shule, wavulana wakiwa 4,806 na wasichana 4,917 katika wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa. Kwa kipindi hicho (2010-2016) wavulana 2,991 waliacha masomo na wasichana 2971, kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoro, kuhama, kupata mimba na ndoa za utotoni.

Amesema kuwa kufuatia taarifa iliyotolewa na gazeti hilo sio za kweli na kwamba limetumia takwimu ambazo sio sahihi kwa wasichana hivyo kuwataka wananchi kutoziamini kwakuwa zinapotosha jamii.

“Shabaha kuu za Serikali nchini ni kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na kupata mimba kwa asilimia 50  ifikapo Juni 2022, kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi asilimia 5, na kuongeza msaada wa kielimu kwa wasichana wanaotoka katika familia maskini kutoka asilimia 23.4 hadi asilimia 53.4,”amesema Siyame

Mahakama nchini Kenya yapingana na Tume ya Uchaguzi IEBC, yatoa maamuzi haya
Lyaniva awafunda wakurugenzi Dar, awapa mbinu za kupambana na uhalifu