Serikali imekanusha tangazo linalosambazwa  kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari “Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000”, likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbali mbali wa Serikalini.

Akikanusha tangazo hilo Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Xavier Daudi amesema taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wanapaswa kuipuuza taarifa hiyo.

Katibu amesema kuwa matangazo yote yanayotolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajra lazima yaonekane kwenye tovuti Sekretarieti ya Ajira ya www.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.

Amesema kama inavyofahamika kuwa Serikali imetoa taarifa ya kusitisha ajira mpya Serikalini kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa, hivyo kwa kuwa zoezi hilo bado halijakamilika amewaomba wananchi wote na wadau wa Sekretarieti ya ajita kuendelea kuvuta subira hadi pale zoezi litakapokamilika na taarifa itatolewa rasmi na mamlaka husika.

Sekretarieti ya Ajira pia imewaomba wananchi na wadau wote wanapoona matangazo ya kazi yanayodaiwa kutolewa na Sekretarieti ya Ajita wajiridhishe kwa kuangalia katika tovuti portal ya Sekretarieti ya Ajira kabla ya kuyafanyia kazi.

Nape Atema Cheche, Atangaza Kiama Kwa Walanguzi Wa Kadi
Majaliwa apokea jumla ya sh. mil.190 kutoka Pakistani na wengine, Tetemeko Kagera