Serikali ya awamu ya Tano imeendelea kutafuta namna ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma ambapo sasa imegeukia suala la uchapishaji wa kadi za kupeana heri ya Christmas na Mwaka Mpya.

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson msigwa, imeeleza kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi hizo kwa gharama za serikali .

Balozi Sefue ameeleza kuwa taasisi/mtu yeyote atakayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.

Ameagiza kuwa fedha zilizokuwa zimetengwa na taasisi kwa ajili ya kazi hiyo zitumike kufanya shughuli nyingine ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ambayo taasisi husika inadaiwa na wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao.

Diamond atajwa kati ya watu 100 Afrika wenye sifa hizi
Chadema, Familia ya Mawazo yashinda Kesi dhidi ya Polisi, Mawazo Kuagwa Mwanza