Serikali ya Sudan Kusini imejiondoa kwenye mazungumzo ya amani na makundi ya waasi, ikitoa shutuma kuwa yana lengo la kupoteza muda na ni matayarisho ya kujiandaa kwa vita.

Waziri anayeshughulikia masuala ya rais, Marial Benjamin ameyasema hayo na kudai kuwa Serikali ya Sudan Kusini imeamua kusitisha ushiriki wake katika mazungumzo ya amani ya Roma kwa muda usiojulikana.

Moja kati ya vikao vya Serikali ya Sudan vya kutafuta amani. Picha ya Zacharia Abubeker / AFP

Mazungumzo hayo, kati ya serikali na muungano wa makundi ya waasi ambayo hayakutia saini makubaliano ya amani ya mwaka 2018, yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe, yalisimamiwa mjini Roma na shirika moja la kikatoliki lililo na mafungamano na Vatican.

Hata hivyo, mazungumzo hayo, pia yalianza mwaka 2019 lakini machafuko bado yanaendelea katika eneo la kusini mwa nchi hiyo, licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha vita mapema Januari 2020.

Nyerere na Tambo ndani ya ofisi ya ukombozi
Rais ateta na akinamama wa vijana wapiganaji