Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kujiepusha na rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kutenda haki kwa wananchi na watumishi walio chini yao, kuwahudumia wananchi kwa staha, kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo hii leo Machi 13, 2023 wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo katika mji wa Serikali, Mtumba.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Amesema, Wakuu hao wa Wilaya pia wanatakiwa kusimamia suala la uhifadhi wa vyanzo vya maji na matumizi ya nishati mbadala, ili kupunguza utegemezi mkubwa wa kuni na mkaa huku akiwasisitiza suala kuwa makini wanapozungumza na Umma kwa kuhakikisha wanatumia lugha fasaha.

Awali, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo aliwataka Wakuu hao wa Wilaya kusimamia kikamilifu suala la migogoro ya ardhi, na migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo inasababishwa na viongozi katika maeneo husika kwa kutotimiza wajibu wao kikamilifu.

Arteta amjibu kimafumbo Pep Guardiola
Nyama ya Kasa yauwa watu saba Mafia