Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amewaagiza Viongozi wa ngazi za Shehia ,Wilaya na Mkoa Kisiwani Pemba kulidhibiti wimbi la wizi wa mazao na mifugo hasa katika kuelekea kipindi cha mfungo wa ramadhani na siku kuu, hali inayoathiri uchumi na juhudi za Wananchi kimaendeleo.

Othman ameyasema hayo wakati akizungunza na Masheha, Viongozi wa Baraza la mjini na watumsihi wa ngazi mbalimbali wa Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika ziara ya kuelezea mpango wa Serikali wa kuirejesha na kurithisha Zanzibar ya kijani.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman. (kulia)

Amesema, tatizo la wizi wa mifugo na mazao ya wakulima limeshamiri sana kisiwani humo katika kipindi hiki kisiwani humo hasa kwa baadhi ya shehia ambapo inatokea kwamba ngombe wawili wa mtu moja kuibwa kwa siku moja.

Aidham, amewataka Viongozi wa ngazi za Shehia wakiwemo na Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha wanashirikiana na vyombo vya ulinzi kukomesha suala hilo, ili lisiendelee kuwaumiza wananchi na hasa wafugaji na wakulima.

Ahmed Ally: Tunazungumzwa kama tumefungwa
Chris Sutton amkataa Bruno Fernandes Man Utd