Utekelezaji wa agizo la serikali la ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) umeonekana kutoiridhisha serikali.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameeleza kutoridhishwa na utekelezaji huo na kueleza kuwa nyumba zinazojengwa na shirika hilo hivi sasa sio za gharama nafuu kama inavyoelezwa kwa kuwa mwananchi wa kipato cha chini hawezi kumudu gharama zake.

Lukuvi aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na viongozi wa shirika hilo katika Mkoa wa Tanga. Aliwataka kuwatumia wataalam wao kutathmini jinsi ya kujenga nyumba zinazoweza kuwa na gharama nafuu ambazo mtu wa chini atazimudu katika uhalisia.

“Ninyi viongozi hamtapimwa uwezo wenu kwa kujena majumba mengi. Mtapimwa kwa jinsi mtakavyotekeleza agizo hili. Nyumba za gharama nafuu tunataka ziwe za gharama nafuu kweli na sio longolongo. Huu ndio mtihani wenu, mkishindwa hamna chenu,” alisema Lukuvi.

Naye Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Tanga alimueleza Waziri Lukuvi kuwa shirika hilo limekamilisha mpango wa kujenga nyumba za bei nafuu katika wilaya ya Mkinga na kwamba itajenga nyumba na kuziuza kwa wananchi kwa gharama ya shilingi milioni 40 kwa kima cha chini.

AT amuandikia ujumbe mzito Ali Kiba, afichua mengi kati yao
Maafande Wa Ruvu Shooting Warejea Ligi Kuu