Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari..

Taarifa za mbunge huyo, zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Daniel Masolwa, pamija na Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella wlipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,

Amesema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonyesha kuwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi.

“Napenda kukanusha kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za Pato la Taifa zimepikwa, Mh. Zitto anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za Pato la Taifa ni ya kitaalam na inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu na Shirika la Fedha Duniani (IMF)”,amesema Masolwa

Aidha, ameongeza kuwa miongozo hiyo ni pamoja na mifumo ya pato la Taifa ya mwaka 2003 na 2008 na mwongozo wa kuainisha shughuli za kiuchumi Toleo la Nne ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2016 Tanzania imekuwa nchi ya pili kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kwa utoaji, uchambuzi, usimamizi na usambazaji wa takwimu  kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella amesema kuwa Mh. Zitto amekokotoa ukuaji wa Pato la Taifa anaodai kuwa ni sahihi kwa kuangalia tofauti kati ya ongezeko la ujazi wa fedha na mfumuko wa bei jambo ambalo sio sahihi kulitumia kama kipimo.

Video: Kangi Lugola azindua operesheni ya usafi wa mazingira
Mdee amnong'oneza Nyalandu kinachoendelea Chadema