Kufuatia kuwepo kwa wingu zito lililokuwa limetanda kuhusu hatua ambazo zilikuwa zimeanza kuchukuliwa na Serikali dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vinaikosoa katika utekelezaji wake katika majukumu mbalimbali.

Serikali imesema kuwa hakuna chombo chochote cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kuandika habari zenye mrengo wa kukosoa sera na utekelezaji wake kama ambavyo wadau wengi wamekuwa wakiaminisha umma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi wakati akizungumza katika Kipindi cha Habari Kuu kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Startv mjini Dodoma.

Amesema kuwa Sheria na 12 ya huduma za habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51 kinatoa ruhusa kwa chombo cha habari kukosoa kwa lengo la kuonyesha njia mbadala katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

“Hakuna chombo cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kukosoa, haki hiyo ipo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51, tutaendelea kuthamini na kufanyia kazi ukosoaji huo,” Amesema Dkt. Abbasi.

Hata hivyo Dkt. Abbasi amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa chombo kitakachokiuka sheria na misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa.

 

AS Monaco Yamnasa Soualiho Meite
Picha: Angalia Safari Ya Mwisho Ya Cheick Tiote

Comments

comments