Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya Watanzania wenye tabia ya uvivu na kupenda kubweteka bila kujituma, huku akisema wakati wa utawala wake hakutakuwa na vitu vya bure.
 
Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga waliohudhuria uzinduzi wa kituo cha mabasi (Stand) wilayani humo, na kusema kuwa watu wanaopenda kukaa vijiweni bila kujishugulisha huku wakilalamika njaa na hakuna pesa, ni bora wafe na njaa
 
” Wakati wa kukaa kwenye magenge na kupiga maneno umepitwa na wakati, mnakaa kwenye pool unasubiri vitakuja hakuna, vya namna hiyo nataka kuwaeleza havitakuja kwenye utawala wangu, mnakaa mnasubiri tuna njaa tunataka mtuletee, mimi njaa nafuu ikuue kuliko nikuletee chakula, kwa sababu kama mwenzako ana chakula wewe una njaa, hatuwezi tukavumilia vitu vya namna hiyo”, amesema Rais Magufuli   
 
Aidha, ameongeza kuwa ni lazima aeleze ukweli hata kama kuna baadhi watamchukia amesema kuwa atasimamia msimamo wake huo wa kusema kweli kwani lengo lake ni kutaka Tanzania isonge mbele.
Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa Serikali inalengo kubwa la kuwasaidia wananchi hivyo watoe ushirikiano ili kuweza kutatua kero mbalimbali zinazo ikabili Jamii ya Watanzania

Singida Utd Wafunga Dirisha La Usajili Kwa Kushusha Kifaa
Mzee wa Upako amvutia Q-chief