Serikali imesema kuwa imetenga sh.bilioni1.669 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika wilaya ya Ileje mkoani Songwe ili kuweza kuwaondolea kero ya maji wananchi.

Hayo yamesema mapema hii leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Itumba, ambapo amesema kuwa kati ya fedha hizo sh. bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji miwili ya Isongole na Itumba wilayani Ileje.

“Kiasi kingine cha shil. milioni 669 kimetengwa kwa ajili ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ileje katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Kampeni ya Rais Dkt. Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji kwa urahisi,”amesema Majaliwa

Aidha, Majaliwa amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400. huku akiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe kuhakikisha inaimarisha ulinzi katika maeneo ya mipaka.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kamati hiyo inatakiwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka ili kuizua wageni kuingia bila ya kufuata taratibu zilizowekwa kisheria na kuweza kuzuia uhalifu ambao unaweza jitokeza.

 

Lukuvi awaweka kikaangoni maafisa Ardhi na Mipango
LIVE: Rais Magufuli katika ziara mkoani Kigoma