Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (NASA) umempa masaa 72 Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini humo, Keriako Tobiko kuwafungulia mashtaka maafisa wa IEBC wanaotuhumiwa kuharibu uchaguzi uliofanyika Agosti 8 mwaka huu.

Muungano huo wa vyama vya siasa nchini humo umesema kuwa mahakama ya juu siku ya Jumatano haikuwaondolea lawama maafisa wa IEBC na kwamba ni lazima washtakiwe kwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.

”Kufuatia uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu, tunaangalia uwezekano wa kuwafungulia mashtaka wale woote waliosababisha kuuvuruga uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu, hivyo tunaipa serikali masaa 72 iwe imewafungulia mashtaka maafisa wa IEBC, amesema Mbunge Mathare, Anthony Olouch

Aidha, amesema kuwa uchunguzi kuhusu uhalifu uliotekelezwa na maafisa hao ufanywe mara moja kisha wafunguliwe mashtaka kwani kitendo walichokifanya si cha kiungwa hata kidogo.

Hata hivyo, Olouch amewataja Maafisa wa IEBC ambao NASA inataka wafunguliwe mashtaka ni pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu, Ezra Chiloba, Mwenyekiti Wafula Chebukati, Betty Nyabuto, Immaculate Kassait, James Muhati, Praxedes Tororey ambaye amejiuzulu, Moses Kipkogei, Abdi Guliye, Molu Boya na Marjan Marjan.

Mbowe ashangazwa na kauli ya Waziri Ummy, Spika
Mpina atoa maagizo kiwanda cha Azania