Serikali imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa vivuko viwili vya MV Athor na MV Orion vinavyofanya kazi kutoka Mwanza mjini kuelekea wilayani Sengerema mkoani Mwanza, baada ya kubainika kuwa na mapungufu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa zoezi hilo linaanza leo Juni 12, 2021 ambapo amesema wakuu wa mkoa na wilaya wasiingilie maamuzi hayo.

Amesema kuwa awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.

Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine, pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma.

Msaidizi wa ndani auwa mama na watoto wake wawili
Rais Samia asimulia picha alizooneshwa madaktari wakiwa ‘hoi’