Serikali imekiri kuwa askari wa wanyamapori huwa wanakamata wananchi katika Hifadhi ya Serengeti kufuatia ukweli kwamba wananchi hao huingia kwenye hifadhi hiyo bila kufuata utaratibu maalumu.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akijibu swali la mbunge wa Serengeti, (Chadema), Marwa Chacha ambapo amesema kuwa mpaka sasa kuna kesi 437 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za usikilizwaji.

Amesema kuwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imepakana na wilaya nane tofauti tofauti hivyo anapokamatwa mtu ndani ya hifadhi hiyo hupelekwa katika kituo cha polisi kilicho jirani kwa hatua zaidi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa baadhi ya watuhumiwa ambao wamekuwa wakikamatwa wengi wao wamekuwa wakijihujihusisha na masuala ya uhalifu ndani ya hifadhi hiyo.

 

 

 

Video: Bajeti ya upinzani kaa la moto, Mradi mpya wa maji wasomba vigogo Dawasa
Atletico Madrid wafanya umafia kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa