Waziri wa Afya , maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu amethibitisha kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na virusi vya Covid 19 ambao umetolewa na bilionea wa China Jack Ma.

Waziri Ummy amesema kuwa vifaa hivyo vimewasili uwanja wa ndege jana Machi 24, usiku, na ametoa shukurani wa Jack Ma pamoja na serikali ya Ethiopia iliyofanikisha usafirishaji wa vifaa hivyo.

Jana waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali alisema tayari mchana wa jana vifaa vya kujikinga na corona vilivyotolewa na Bilionea wa China Jack Ma na Alibaba Foundation vimesafirishwa kuja Tanzania pia Somalia.

Hali kadhalika vifaa vilisafirishwa pia kwenda Nchi nyingine 9 ikiwemo Kenya, zimo mask, vifaa vya kupimia na nguo za kujikinga na corona.

Hadi sasa wagonjwa walioambukizwa virusi nchini Tanzania ni 12, huku dunia nzima waathirika wakiwa 303,525, vifo vikiwa vimefikia 19, 607 na waliopona wakiwa 111, 870.

Mtoto wa Malkia Elizabeth aambukizwa Corona
Mara: Wahamiaji haramu wakutwa na vitambulisho vya taifa

Comments

comments