Serikali imefanikiwa kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani kupitia sheria ya huduma kwa jamii Sura ya 291, Sheria ya Majaribio na Ujenzi wa Tabia sura ya 247 na Sheria ya Magereza sura ya 34/1967, kifungu cha 52.

Kwa mujibu wa Sheria hiyo wafungwa waliohukumiwa vifungo visivyozidi miaka mitatu hutumikia adhabu nje ya magereza.

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za uangalizi katika Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi ambaye ni katibu wa kamati ya taifa ya huduma kwa jamii Alloyce Musika ameeleza hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo katika kikao cha kamati ya idara hiyo, kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa TANAPA, jijini Dodoma.

“Lengo la kuanzishwa kwa idara hii ni kuipunguzia serikali gharama za kuhudumia wafungwa magerezani, kudhibiti tatizo la urudiwaji uhalifu, kupunguzwa msongamano wa wafungwa magerezani, hadi kufikia Novemba 30, 2020,  wafungwa 1781 walikuwa wanaendelea kutumikia adhabu za nje ya gereza, wafungwa 1447 walimaliza kutumikia adhabu zao,” amesema Musika.

“Dira yetu ni kuwa chombo kinachozingatia weledi, taratibu, vigezo vya kitaifa na kimataifa katika urekebishaji wahalifu ndani ya jamii,”ameongeza Musika.

Aidha,  kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Huduma kwa Jamii Jaji Zephrine Galeba iendelee kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.

Chanzo kifo cha Askofu Banzi
Hatma ya Mdee na wenzake kufahamika Desemba 27