Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameruhusu Wafanyabiashara wa Soko la Karume kurejea na kuendelea na Biashara kwa kuwekewa Mpango mzuri.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wakati wa mkutano wa hadhara na wafanyabiashara wa soko la karume mara Baada ya kupokea Taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo Cha Moto.

Rc Makalla amesema Rais Samia ameelekeza uwepo utaratibu mzuri wa kuzuia Moto, kuhakikisha hakuna atakaedhulumiwa eneo lake na kutoa ruhusa kwa Wafanyabiashara kujenga Vibanda kwa gharama zao.

Kuhusu Ripoti ya chanzo Cha Moto, RC Makalla amesema Kamati imebaini Moto huo ulitokana na Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya “Mateja”.

Aidha RC Makalla amesema Baada ya kupokea ripoti hiyo ataikabidhi kwenye Mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji wa maoni na Mapendekezo yote ya Kamati.

Miongoni mwa Maoni na Mapendekezo ya Kamati hiyo ni pamoja Ujenzi wa soko jipya linaloendana na ali ya Sasa na vizimba kutolewa kwa kipaombele kwa wazawa, uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia Moto, barabara za kuingia na kutoka, Ujenzi wa Majengo ya Muda mfupi, Kila mfanyabiashara kuwa na bima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na Kuungua Hilo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 7.2 ambapo idadi ya Wafanyabiashara waliokumbwa na janga Hilo Ni 3,090.

Marafiki wa DJ aliyejiua kwa sumu wafunguka chanzo
TCRA yafunga kipindi cha efatha ministry