Watoto wa mitaani 6,393 kutoka mikoa 6 Tanzania wametambuliwa na Wizara ya Afya na kupatiwa huduma mbalimali zikiwemo afya, malazi, elimu pamoja na msaada wa kisaikolojia na wizara hiyo. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa afya Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge Fakharia Shomary Khamis aliyehoji hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na ongezeko la watoto wa mitaani.

Amesema watoto hao, wa kiume 4,865 na wa kike 1,528 wanatoka katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Iringa, Arusha, Dodoma na Mbeya, ambapo ametaja sababu zinazopelekea ongezeko hilo kuwa ni pamoja na vifo vya wazazi, unyanyasaji na umasikini

Ndugulile amesema Serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa malezi na ulinzi wa watoto na kutoa wito kwa jamii kuwajibika katika matunzo, malezi na ulinzi wa watoto.

Tanzania kitovu cha idadi ya Simba duniani
Hamann amkataa Leroy Sane, ampigia chepuo Milot Rashica