Serikali imesema kuanzia sasa hakuna dalali atakayeendesha shughuli za udalali bila kusajiliwa na kuwa na leseni.

Agizo hilo limetolewa na katibu mkuu, wizara ya fedha na mipango, Dotto James wakati akizindua mfumo wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji minada kwa njia ya kielektroniki uliofanyika jijini Dar es salaam.

Amesema tayari shughuli hizo ni rasmi na wanaotakiwa kuziendesha ni waliosajiliwa pekee na kwamba wamejipanga kuanza kufanya operesheni katika kila mtaa.

” kama unajiita dalali na unafanya shughuli hizo bila kujisajili, mwisho wako umefika, serikali tuna mbinu mbalimbali za kufanya shughuli zetu, tutapita huko mitaani kwenu tutawakamata na hatutakuwa na huruma tutakutana nao mahakamani kisutu” amesema James.

Na kuongeza kuwa ” wametapeli watu kwa muda mrefu, wamesababisha hata wale waaminifu ambao wamejisajili na kulipa kodi Serikalini nao waonekane matapeli, ilifika wakati hata kwenye familia mtu mmoja akiwa dalali familia yote inadharaulika”.

Katika uzinduzi huo katibu mku amesema usajili kwa sasa umerahisishwa na kwamba watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia kompyuta au simu za mkononi katika mikoa wanayoishi badala ya kusafiri mpaka Dodoma kama ilivyokuwa zamani.

Bashiru: Katiba mpya ni ajenda ya kudumu
Angalia ratiba ya CHAN 2020