Serikali nchini, imezikumbusha Mamlaka za Elimu kuhakikisha utoaji wa adhabu Shuleni unazingatia waraka namba 24 wa mwaka 2002, ambao umeainisha utaratibu wa utoaji wa adhabu huku ikisema utaratibu uliotolewa kwenye waraka huo ni pamoja na adhabu kuzingatia ukubwa wa kosa, jinsia, afya ya Mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Ufafanuzi huo, umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitoa ufafanuzi na mwelekeo wa Serikali kuhusu changamoto ya nidhamu, malezi na adhabu zinazotolewa Shuleni, ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa taarifa zenye kuonesha matukio ya adhabu zinazotafakarisha dhidi ya Watoto katika Jamii na Shuleni, Bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, Mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko mkononi na Mwalimu wa kike isipokuwa kama Shule hiyo haina Mwalimu wa kike, adhabu ya viboko itakapotolewa iorodheshwe katika kitabu kilichotengwa kwa kuonesha jina la Mwanafunzi, kosa alilotenda, idadi ya viboko na jina la Mwalimu aliyetoa adhabu.

Hata hivyo, Majaliwa pia ametoa wito kwa wahanga kuwasilisha taarifa kwa Mamlaka husika na sio kurusha kupitia mitandao ya kijamii, jambo ambalo linaweza kuleta taharuki, kuleta uhasama na chuki ndani ya Jamii.

Bares: Tutashirikiana kuinusuru Prisons
Robertinho aanika ramani ya Ubingwa