Serikali ya Tanzania imesema kuwa, itasitisha kwa muda safari za Ndege yake aina ya Airbus A22O- 300, iliyokuwa inashikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama ambapo jana iliachiwa,  kufuatia hali ya vurugu na machafuko yanayoendelea nchini humo.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 05, 2019 na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe wakati wa Uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

”Kwa mujibu wa ratiba, kesho Ndege yetu ilikuwa inatakiwa iruke kurudi Afrika ya Kusini, lakini ninyi ni mashahidi kwamba nchi ile kuna fujo kubwa inaendelea, kwahiyo tumeona kwamba hatuwezi kuwapeleka abiria eneo ambalo tunajua maisha yao yako hatarini, tunaomba muendelee kuvuta subra,” amesema Waziri Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe ameongeza kuwa safari hizo zitasitishwa hadi Serikali itakapofanya mawasIliano na Serikali ya Afrika ya Kusini ili kuhakikisha kwamba unakuwepo usalama wa chombo na abiria, ambapo safari hizo zitarudi tena endapo watapokea barua ya kuwahakikishia ulinzi wawapo nchini humo bila madhara yoyote.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 6, 2019
Nigeria yatuma ndege nne Afrika Kusini