Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka mamlaka na taasisi zinazohusika na usimamizi wa bima na hifadhi ya jamii barani Afrika, zitoe elimu ya kutosha kwa jamii, ili watu wajiunge na huduma hizo.

Majaliwa, ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa Mamlaka za Bima barani Afrika jijini Arusha, uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali Afrika.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri wa Fedha Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba

Amesema, “Mamlaka na taasisi zetu zinazohusika na usimamizi wa bima na hifadhi ya jamii ongezeni juhudi ya utoaji wa elimu ya bima na hifadhi ya jamii barani Afrika kwa namna ile ambayo nchi husika itaona inafaa.”

Kuhusu makubaliano ya kuwa na eneo huru la biashara kwa bara la Afrika, (African Continental Free Trade Area), Waziri Mkuu amesema utiaji saini wa utekelezaji wa makubaliano hayo ulifanyika Januari mosi, 2021 na sekretariati yake ipo jijini Accra, nchini Ghana.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa  wa Wakuu wa Mamlaka za Bima Afrika wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano huo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC), jijini Arusha.

Aidha, amewataka wataalamu hao waangalie namna ya kuifanya mifumo ya hifadhi ya jamii na pensheni iwe shirikishi kwa watu wote na hasa kuwapa kipaumbele wanawake, vijana, wazee na wakulima ambao wako katika mazingira magumu.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alisema eneo la bima lilishatolewa maelekezo na Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 22, 2021 wakati alipohutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

Mfumuko wa bei 'kaa la moto' kwa jamii
Pendekezo la kumshitaki Rais kuwasilishwa Bungeni