Serikali imeombwa kuboresha miundombinu na mazingira kwa ujumla pamoja na kutoa elimu katika vituo vya mabasi yaendayo kasi na jinsi ya kuutumia mradi huo mpya jijini Dar es Salaam.

Wakifanya mahojiano na Dar24 watumiaji wa mabasi yaendayo kasi kwa nyakati tofauti tofauti wamesema serikali inatakiwa kuwatumia wasanii na watu mbalimbali maarufu katika kutoa elimu na uhamasishaji wa kutunza mazingira ya mradi huo

Bw. Elisante Urassa mkazi wa Kimara amesema kama jinsi serikali ilivyo buni mradi huo pia inatakiwa kuandaa mikakati mbalimbali ya kuboresha na kuutunza mradi huo ambao bado ni mgeni kwa Tanzania pia kuweka vibao mbalimbali vya maelekezo ya jinsi ya kutumia mradi huo na kujenga vyoo vya wasafiri pamoja na kuongeza madirisha ya kukatia tiketi kwa baadhi ya vituo.

Hata hivyo Mama Omari mkazi wa kimara amewashauri wasafiri kutumia usafiri huo wa haraka ili kuiunga serikali mkono kwa kutumia mabasi yaendayo kasi ili kuimarisha mradi huo mchanga.

Akizungumzia suala la siku ya leo jumatatu wananchi kuwa wachache katika mabasi hayo Mama Omari anafafanua kwamba wasafiri wengi wanaona bora kutumia muda mrefu kuliko kutoa pesa nyingi na kufika mapema waendapo na kuongeza kwamba nauli za mabasi ya kawaida na mradi huo hazijapishana sana

Akiwasilisha kero yake kwa Dar 24 Bw. Kasian Mrisho amesema kuwa magari hayo yana spika kwa ndani hivyo dereva anatakiwa kutaja vituo kwani abira wageni wanapata tabu kwa kutokujua maeneo ya kushukia

Happy mkazi wa kimara amesema usafiri kwa upande wa kimara morocco ni wa tabu kidogo kwani ametumia zaidi ya saa moja kusubiri usafiri huu ambao magari yake yamekua machache kutokana na uchache wa abiria katika siku ya leo ofauti na Alvin ambaye amesema kwa sasa mradi huu unatakiwa kupewa muda kwani ndo kwanza umeanza kutoa huduma.

Hili hapa Daraja la Jipya la Morocco

Makamu wa Rais awasha moto, awapa ‘dedilaini’ wakuu wa Mikoa na Wilaya
Profesa Muhogo amnyamazisha Mchungaji Msigwa kuhusu fedha za MCC