Serikali imetangaza rasmi kuzitambua dawa tano zilizotengenezwa kiasili  baada ya kukaguliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali na kuthibitishwa kuwa zinatibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo dawa ya Ujana inayotibu nguvu za kiume.

Dawa hizo zimetangazwa leo, jumanne Machi 13, 2018 na Msajili wa Baraza la Tiba za Asili na Mbadala, Dk Ruth Suza katika mkutano na waandishi wa Habari.

Amezitaja dawa hizo kuwa ni Ujana, IH Moon, Coloidal Silver, Sudhi na Vatari zinazotibu magonjwa mbalimbali.

Dk Suza amesema walikitumia  kitengo cha Boring cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kupitia Mkemia Mkuu wa Serikali.

Naibu waziri wa Afya Dk Faustine Ndugulile ametoa agizo kwa waganga wote wa tiba asili na tiba mbadala kuacha mara moja kutoa matangazo yao mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mabango ya barabarani.

‘’Nawataka waganga wote kujiepusha na matangazo yanayokinzana na sheria, kanuni na taratibu ikiwa ni pamoja na kuondoa mabango yaliyozagaa mitaani yanayoonyesha magonjwa mbalimbali kama Ukimwi na matangazo mengine,’’. Amesema Ndugulile.

Aidha Dk Ndugulile amekemea wale wote wenye mashine aina za Quantum kuacha mara moja kuzitumia kwa kuwadanganya wananchi kuwa zinaondoa sumu mwilini.

Tshishimbi awapiku Okwi, Buswita
Rais Kiir amtimua waziri wa fedha na ofisa wa jeshi