Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 23.061 kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya miradi ya matengenezo mbalimbali ya barabara mkoani Pwani katika kipindi cha mwaka 2018/2019 .

Hayo yamesemwa mjini Kibaha mkoani Pwani na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Yudas Msangi wakati wa kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo.

Amesema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 14 zitatumika kutengeneza barabara zinazounganisha maeneo muhimu ya kiuchumi ili kurahisisha mawasiliano kwenye maeneo hayo.

“Matengenezo ya kawaida ya lami yametengewa shilingi bilioni 3.1, matengenezo maalumu lami kilometa 15.6 yametengewa kiasi cha shilingi bilioni 7 huku matengenezo ya sehemu korofi 0.7 kilometa yametengewa kiasi cha shilingi milioni 57.9,”amesema Msangi.

Aidha, amesema kuwa matengenezo madogo madogo ya madaraja 23 yametengewa kiasi cha shilingi milioni 74 na matengenezo makubwa ya madaraja mawili yametenegewa kiasi cha shilingi milioni 200.4.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarist Ndikilo ,amesema kuwa katika kuelekea kwenye ukanda wa viwanda ,ni lazima miundo mbinu ya barabara iboreshwe na kujengwa ili kuvutia wawekezaji.

Netanyahu aingia matatani, wapinzani wamtaka ajiuzulu
Video: Maalim Seif ana dharau ndio maana tumefikia hapa -Sakaya