Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Mjaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 15 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana zaidi 2,500 ili kuwajengea uwezo waweze kushiriki kama nguvu kazi kwenye viwanda vinavyotarajiwa kujengwa nchini.

Majaliwa amesema hayo Desemba 8, 2016 kwenye sherehe za utoaji wa tuzo ya muajiri bora wa mwaka 2016, zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania, na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Tuzo hizo zimeandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

Majaliwa alisema Serikali imeanza kujielekeza katika kutoa mafunzo kwenye sekta za kipaumbele kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kama kilimo biashara, mafuta, gesi, utalii, usafirishaji, ushonaji na bidhaa za ngozi.

Pia, amesema jitihada zinaendelea kwenye maeneo mengine ili waajiri wawe na wigo mpana wa kuwapata wafanyakazi wenye stadi stahiki kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wao kuwa nguvu kazi yenye ujuzi na umahiri mkubwa kwa lengo la kuongeza tija.

 

Mwita: Tunaendelea na ukukarabati wa stendi kuu ya ubungo
Tendwa: Vyama vingi vilitokana na vuguvugu la wananchi