Maafisa wa ngazi ya juu wa Serikali ya Uganda, wamesema wameaarifiwa kuhusu uwepo wa tukio la kurekodiwa kwa kisa kimoja cha ugonjwa wa Ebola, kilichotokea katika Wilaya ya Mubende ya kati nchini humo, huku wakisema mtu mmoja inasadikika kuwa amefariki kutokana na maradhi hayo.

Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng amesema mlipuko wa ugonjwa huo ambao unachukuliwa kuwa nyeti kwa sababu ya uwezekano wa kuathiri sekta ya utalii, amelitolewa hii leo asubuhi Septemba 20, 2022 na kwamba taarifa za awali zilimfikia Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Amesema, “Uganda inathibitisha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola (EVD) katika Wilaya ya Mubende, Uganda na kesi iliyothibitishwa ni ya mwanamume mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Ngabano kata ndogo ya Madudu Wilayani Mubende aliyeonyeshwa dalili za EVD na baadaye alifariki.”

Wahudumu wa Afya wakibeba mwili wa mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Ebola. Picha na ABC News.

Waziri Ruth ameongeza kuwa, “Wafanyikazi wakuu wa Wizara ya Afya walikimbilia Mubende baada ya idadi isiyojulikana ya wakaazi wa eneo hilo kuugua kile kilichoripotiwa kama wana dalili za ugonjwa wa kushangaza na baada ya vipimo hapo jana ulipatikana uthibitisho ambao sasa tunaujulisha umma.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ni jirani na Uganda upande wa magharibi, kwa sasa inapambana na mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Ebola, ambao hapo awali ulitajwa kama ni homa ya kuvuja damu huku Shirika la Afya Duniani (WHO), likisema ugonjwa huo huambukizwa kwa watu kutoka kwa wanyama na huenea kwa njia ya maambukizi.

Nchi ya Uganda, imekuwa na angalau matukio matatu ya awali ya Ugonjwa wa Ebola, ambayo inaripotiwa kuwa hapo awali ilikuwa na hali mbaya zaidi kwa mwaka 2000, na inasemekana maradhi hayo yaliua mamia ya watu, akiwemo mtaalamu wa matibabu, Dkt. Matthew Lukwiya.

Ally Mayay ateuliwa Kaimu Mkurugenzi wa Michezo
Hassan Mwakinyo: Watanzania punguzeni mihemko