Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amewasilisha mapendekezo ya serikali ya mpango wa maendeleo wa taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2019/20.

Amesema kuwa serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo huku kati ya fedha hizo shilingi trilioni 20.5 zikitengwa kwa matumizi ya kawaida ikijumuisha gharama za uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020.

Amesema kuwa gharama za matumizi ya maendeleo zinatarajiwa kuwa shilingi trilioni 12.4  ambapo kati ya hizo, shilingi trillion 9.3 ni fedha za mapato ya ndani na trilioni 2.1 ni za nje.

Kwa upande wake Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya uwasilishaji huo amewataka mawaziri wote kuhakikisha wanahudhuria vikao vya kamati za bunge hasa pale wanapohitajika ili kuweza kutoa ushirikiano katika uboreshaji wa bajeti.

Aidha, baadhi ya wabunge pia wamezungumzia mapendekezo hayo baada ya Waziri Mpango kuwasilisha mpango huo, ambapo wameeleza jinsi bajeti hiyo ilivyo kuwa na changamoto ambazo zinahitaji kutatuliwa kabla ya kukamilishwa kwake.

 

 

Video: Mbowe, Matiko wawa kivutio mjengoni, Uchaguzi, matumizi kugharimu tril. 21
TID awatolea uvivu wasanii, ‘watoto wanakuwa mashangingi’